KUOMBA KWENYE LANGO LA USIKU

| Makala

MAOMBI YA USIKU WA MANANE

       {MIDNIGHT PRAYERS}

00:00am - 01:00 am {EAT}

Bwana Yesu asifiwe sana mtu wa Mungu, nakumbuka nilikufahamisha kwa habari ya mabadiliko ya ibada zetu za maombi ya LIVE kwenye Channel yetu ya SIRI ZA BIBLIA Youtube.

Kuanzia ijumaa hii ya tarehe 10/10/2025,maombi yataanza rasmi kufanyika usiku saa SITA mpaka saa SABA.

Huu muda ni lango la mabadilishano ya siku, yaani siku inaisha na inaanza nyingine….katika mazingira kama haya,kuna vitu vya kiroho tunatakiwa kuvizingatia;

Zaburi 119:62 

Usiku wa manane nitaamka nikushukuru, Kwa sababu ya hukumu zako za haki.

Maombolezo 3:22-26 

Ni huruma za BWANA kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu. BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini yeye. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa utulivu.

Ayubu 38:12 

Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza? Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?

Tafadhali zingatia muda wa USIKU {00:00am - 01:00am} namuomba Roho Mtakatifu akupe kibali cha kushiriki kila siku bila kuchoka.

Tuwasiliane kama kuna hitaji lolote unalotaka tumwambie Mungu kwa ajili yako, tuma meseji au voicenote kwa Whatssap namba +255 758 708804

Pastor Innocent Mashauri

Madhabahu ya SIRI ZA BIBLIA

Maarifa ya ki-Mungu

Kuisemesha siku mpya mwanzoni kabisa inapoingia,kuhusu wema na fadhili za Mungu kufuatana nasi kwa masaa yote 24 yanayokuwa mbele yetu.

Kudhibiti maovu yaliyozaliwa kwenye siku inayoisha,ili yasiingie na sisi kwenye siku mpya tunayoipokea

Kumshukuru Mungu kwa siku aliyotupatia,bila kujali imezalisha nini maishani mwako


 SADAKA